- Kaunti ya Makueni imezindua kampuni ya kutengeza maziwa maarufu kama 'Kikima Dairy'

- Kampuni hiyo ilizinduliwa na gavana wa Makueni,Kivutha Kibwana

-Aidha kaunti hiyo pia imeanzisha kampuni ya kutengeneza jusi kutoka kwa matunda aina ya maembe

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana alionyesha furaha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kufanikisha ufunguzi wa kampuni ya kutengeneza maziwa katika kaunti hiyo.

Habari Nyingine: Picha za muuguzi huyu mwenye umbo la malaika zawapa 'mafisi' taabu

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

" Kaunti ya Makueni imejiunga na watengenezaji wengine wa maziwa humu nchini,Kampuni ya Kikima Dairy imekamilika na hivyo basi wananchi watarajie kuuziwa maziwa yenye ladha tamu," Kivutha aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

TUKO.co.ke ilibaini kuwa Kikima Dairy ina uwezo wa kutengeneza na kufungasha zaidi ya lita 300 za maziwa kwa muda wa saa moja na lita 6600 kwa siku.

Maziwa hayo ambayo yamepewa jina" Makueni Fresh' sasa yatauzwa kwenye maduka kadhaa ya jumla.

Habari Nyingine: Cristiano Ronaldo kando, Faiq Bolkiah,19, ndiye mchezaji tajiri zaidi wa soka akiwa na utajiri wa $20 bilioni

Kivutha pia alisema kuwa kaunti hiyo ilizindua kampuni ya kutengeneza jusi kutoka kwa matunda aina ya maemba.

" Huu ni musimu wa maembe katika kaunti ya Makueni,wakulima wamepeleka zaidi ya tani 72 katika kampuni hiyo na wafanyakazi wanatarajiwa kuanza kutengeneza jusi wakati wowote," Kivutha aliongezea.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari am Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia395fpVmopqtnqm2bsXAZqSao6Wau6p52JqdrqaXqq5ut8Cmp66mmWLGonnKrqueppeau6bGwGakmrKZrK5uvMCmpqOZXaOubrbUrKBmsZFiuqKxzJuYZ6Ckork%3D